Wahamasishwa na kuanzisha vikundi 3,62 vya kilimo

18Oct 2021
Na Mwandishi Wetu
Mara
Nipashe
Wahamasishwa na kuanzisha vikundi 3,62 vya kilimo

WAKULIMA wa jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, wameanzisha vikundi 3,62 vya kilimo, kwa ajili ya kurahisha upatikanaji wa huduma kilimo kama pembejeo. mikopo na ushauri wa kitaalamu.

Wakulima wa KIjiji cha Murangi wakiandaa shamba kwa kutumia jembe la kukokotwa na ng'ombe walilopewa na mbunge Prof. Muhongo

Vikundi hivyo viko katika kata 21 zinazounda jimbo hilo, ambapo mkazo mkubwa umewekwa kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia maji ya ziwa Victoria na baadhi ya mito isiyokauka.

Mbunge wa jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo amesema, hatua hiyo pia inalenga kuomngeza kasi ya matumizi ya jembe la kukokotwa na ng'ombe (plau) ambazo litapunguza matumizi ya jembe la mkono.

"Nimeanzisha programu ya kupunguza utumiaji wa jembe la mkono na nimeshagawa majembe 85 ya kukokotwa na ng'ombe katika vikundi 21 na ninahamasisha wakulima kujiunga katika vikundi na hadi sasa vimefikia 362 ambavyo viko kwenye kata zote 21," Prof. Muhongo amesema.

Amesema vikundi hivyo vinachochea maendeleo kupitia kilimo, na kwamba plau inasaidia kuokoa muda wa kazi shambani kwa kutumia kipindi kifupi kwa kulima eneo kubwa kuliko ilivyo kwa jembe la mkono.

"Kutumia plau kusaidia pia kuongeza mavuno na mapato ya fedha kwa wanachama wa vikundi husika na kuwa na uwezo wa kusomesha watoto wao lakini pia kufungua biashara mpya na kukopesha fedha," amesema.

Aidha, kwa niaba ya wakulima wa Musoma Vijijini, mbunge huyo amesema, wakati huu wanapoelekea kwenye kilimo cha trekta, hivyo wanawaomba wadau wa kilimo kuunga mkono ili kuhakikisha vikundi vyote vinapata plau.

"Wanawaomba wadau wa maendeleo kama halmashauri yao kuungana nami kuwagawia plau li kuhakikisha kila kikundi kinakuwa na jembe hilo, kwa ajili ya kupunguza matumizi ya jembe la mkono," amesema.

Habari Kubwa