Akizungumza na waandishi wa habari jana, katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Mbeya, Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Jerome Ngowi, alisema wahamiaji hao walikamatwa juzi katika kizuizi cha magari, Kijiji cha Gari Jembe barabara kuu ya Tanzania na Malawi.
Alisema wahamiaji hao walikuwa wamefichwa kwenye lori aina ya Scania yenye namba za usajili T. 509 AZZ ambalo lilikuwa linaendeshwa na Rabdi Ramadhani (48), mkazi wa Unga Limited, mkoani Arusha.
Alisema maaskari waliokuwapo kwenye kizuizi hicho, walimsimamisha dereva huyo ili wakague gari hilo na walipomhoji kuhusu mizigo aliyobeba alisema amebeba bidhaa za dukani.
Soma zaidi: https://epaper.ippmedia.com