Wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji kumkata mtu koromeo

14Aug 2020
Restuta Damian
Bukoba
Nipashe
Wahukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji kumkata mtu koromeo

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Bukoba, imewahukumu kunyongwa hadi kufa washtakiwa watatu katika matukio mawili ya mauaji na kumwachia huru mmoja miongoni mwao.

Akitoa hukumu ya kwanza inayohusu mauaji, maarufu kama ukataji wa makoromeo, Jaji Sam Rumanyika alisema Aliyuu Dauda na Rashid Athuman, walifanya mauaji ya kukusudia Mei 9, 2015 Kata ya Kitendagulo Manispaa ya Bukoba.

Jaji Rumanyika alisema mtuhumiwa wa kwanza, Dauda, alijihusisha na mauaji ya Herman Grid huko Kitendagulo kwa kumkata koromeo.

Pia alisema mtuhimiwa Athumani alikiri kujihusisha na matukio ya uchomaji wa makanisa.

Jaji Rumayika alisema katika shauri la jinai namba 79/2016, mshitakiwa Shija Bunzali alifanya mauaji ya aliyekuwa Diwani wa Kimwani Wilaya ya Muleba kwa tiketi ya CUF, Sylvester Faustine, Januari 31, 2016.

Alisema mtuhumiwa huyo amehukumiwa kifo baada ya kukiri kuwa vifaa vilivyoko kwake vilivyonekana kuwa na damu ni mali yake.

"Mshtakiwa alikutwa na panga likiwa na damu mbichi na suruali aliyosema ni mali yake ikiwa na tone la damu, kwani taarifa ya vinasaba inatoa vielelezo hivyo," alisema Jaji Rumanyika
Alisema watuhumiwa wawili wa uchomaji makanisa na mauaji wameonekana kuwa na makosa katika kesi ya jinai namba 34/2020 na mtuhimiwa wa tatu kuonekana kuwa na hatia katika shauri la jinai namba 79/2016.

Jaji Rumanyika alisema watuhumiwa hao wawili walikiri mbele ya mlinzi wa amani kuwa ushahidi uliotolewa ulijitosheleza kuwatia hatiani. Ushahidi huo, alisema ulitolewa na ofisa wa polisi.

"Ushahidi uliotolewa na upande mashkata unajitosheleza kuwatia hatiani kwani mashahidi wa watuhumiwa walikuwa watano akiwamo ofisa wa polisi na itoshe kusema kuwa mahakama haiwezi kumtia hatiani mshtakiwa wa upande mmoja tu,” alisema.
Katika hatua nyingine,

Jaji Rumanyika alimwachia huru Ngesela Keeya baada ya vielelezo vya mahakama kutoonyesha kuwa na kosa.

Habari Kubwa