Waumini dini Kiislam wakumbushwa kutenda mema, tahadhari ya corona

24May 2020
Ibrahim Joseph
DODOMA
Nipashe
Waumini dini Kiislam wakumbushwa kutenda mema, tahadhari ya corona

Waumini wa dini ya Kiislamu Nchini wametakiwa kuendeleza mema waliyokuwa wakiyafanya wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani pamoja na kuendelea  kuzingatia maagizo ya kukinga na corona yanatotolewa na viongozi wa Serikali na wataalamu wa afya.

Sheikhe wa msikiti wa Nughe Jijini Dodoma akitoa mawaidha leo mara baada ya swala ya eid el fitri ,swala hiyo huswaliwa baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 24, 2020 na Sheikhe wa Msikiti wa Nughe uliopo Jijini hapa, Sheikhe Omari Salimu Itara akitoa hotuba yake wakati wa  swala ya Eid El Fitri  iliyoswaliwa katika msikitini hapo.

Sheikhe Itara amewataka waaumini wa dini hiyo kuendeleza kufanya mema waliyokuwa wakiyafanya wakati wa  mfungo mwenzi mtukufu wa ramadhani na kuzingatia masharti ya kujikinga na maambukizi ya corona.

 

 

 

 

 

 

PICHA Baadhi ya waumini wa dini ya kiislima Mkoa wa Dodoma wakishiriki kuswali swala ya Eid El Fitri aliyoswaliwa leo asubuhi katika msikiti wa Nughe Jijini Dodoma.

Habari Kubwa