Waitara ameitaka TEMESA kusafisha karakana kuruhusu magari mengine

22Apr 2021
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Waitara ameitaka TEMESA kusafisha karakana kuruhusu magari mengine

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, amewataka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), kuhakikisha wanatoa magari yote yaliyotelekezwa na wamiliki wake katika karakana zote nchini yanayosababisha mrundikano karakana hizo.

Akizungumza na Menejimenti ya Wakala huo, jijini Dodoma, Waitara amesema kuwa hatua hiyo itapelekea kupunguza msongamano katika na kuruhusu magari mengine kupata huduma kiurahisi.

“Magari hapa ni mengi na mrundikano ni mkubwa, mengine yanaonekana ni ya muda mrefu, hakikisheni mnayatoa na kuyapeleka kwa wenyewe ili kupunguza msongamano hapa na hata katika karakana zenu nyingine nchi nzima” amesema Waitara.

“Hakikisheni kuwa mnapunguza gharama, mnatumia muda mfupi na vipuri sahihi katika utengenezaji wenu wa magari, mkifanya hivi mtapunguza malalamiko kutoka kwa washitiri wenu”, amesisitiza Waitara.

Aidha, Waitara ameagiza Wakala huo kuhakikisha wanatafuta njia sahihi ya kuhifadhi mafuta machafu yanayomwagika wakati wa utengenezaji wa magari ili kuhifadhi mazingira katika maeneo yao ya kazi.

Habari Kubwa