Waitara asikitishwa na miundombinu mibovu ya vituo vya usafiri Mpanda

19Dec 2021
Neema Hussein
Katavi
Nipashe Jumapili
Waitara asikitishwa na miundombinu mibovu ya vituo vya usafiri Mpanda

​​​​​​​NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara, ameonesha kusikitishwa na miundombinu chakavu na huduma zinazotolewa kwenye kituo cha usafiri wa treni Mpanda mkoani Katavi Ikiwemo kukosekana kwa jengo la abiria tangu huduma ya usafiri wa treni uanzishwe miaka 50 iliyopita.

Muonekano wa kituo cha Treni Mpanda mkoani Katavi, Kituo hicho hakina jengo la abiria tangu Tanganyika ipate uhuru

Waitara ameyasema hayo jana wakati alipotembelea kituo hicho na kuzungumza na watumishi pamoja na baadhi ya abiria huku akimtaka Mtendaji Mkuu kutoa majibu ni lini jengo la abilia litajengwa.

Waitara amesema pia amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi wanaoishi karibu na reli kutofaahamu mipaka ya reli inapoishia hivyo kupelekea wao kupata usumbufu pindi wanapofanya shughuli zao za kimaendeleo.

"Mi nasema hili jambo halikubaliki na Mh Rais kazi hii hawezi kuipenda tukiacha iendelee kukaa hivi tutakua hatumsaidii hii imenipa picha kuwa kumbe hizi stesheni zote inabidi zikaguliwe inawezekana hali ni mbaya maeneo yote hata usafi tu jengo linanuka utafikili wanalala mbuzi hewa nzito sasa bajeti ya kusafisha tu hapo nikiasi gani hicho?, amesema Waitara.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara akikagua kituo cha Treni Mpanda.

Kwa upande wake Stesheni Masta wa kituo cha Treni Mpanda Emmanuel Mtawali, amesema mabehewa ni machache hasa ya kwenda dare es salaam hivyo kupelekea abiria kulalamika kubanana ndani ya behewa moja pasipokuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona.

"hili tatizo litaboreshwa maana saizi tuna behewa tatu za kwenda dare es salaam kwaiyo hata tukiongezewa mbili zikawa tano zinatosha sana lakini kwa upande wa mabehewa ya mizigo hakuna tatizo," amesema Mtawali.

Baadhi ya abiria wanaotumia usafiri wa treni wamesema kukosekana kwa jengo hilo kunapelekea wao kusimama kwa muda mrefu huku mvua ikiwanyeshea pindi wanapokua kwenye foleni ya kukatiwa tiketi na baadhi ya abiria kulala njee na watoto pindi wanaposubili treni.

Mbali na hayo Naibu Waziri Waitara pia amekagua Uwanja wa Ndege Mpanda na kukili kuwa jengo la abiria ni dogo hiyo ni baada ya kusomewa taarifa fupi kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Ndege Mpanda Jeff Shantiwa.

Muonekano wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mpanda ambalo ni dogo ikilinganisha na wingi wa abiria.

Shantiwa amesema jengo hilo linauwezo wa kuchukua abiria 48 huku ndege inachukua abiria zaidi ya 70 hivyo kupelekea abiria wengine kusimama.

Habari Kubwa