Wajawazito 813,923 wajifungulia vituo vya afya

20Jan 2020
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Wajawazito 813,923 wajifungulia vituo vya afya

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema wajawazito 813,923 sawa na asilimia 74 wamejifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Mwalimu ametoa kauli hiyo leo wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa wizara kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2019 kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii.

Amesema katika kipindi hicho matarajio yalikuwa ni wajawazito 1,100,000 wangejifungua.

"Hata hivyo takwimu zinaonesha kuwa jumla ya wajawazito 813,923 sawa na asilimia 74 walijifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma,"amesema

Aidha, amesema kwa wajawazito walihudhuria kliniki,ni 797,803 sawa na asilimia 73 ya walengwa na walifanya mahudhurio ya kliniki manne na zaidi kama mwongozo ulivyoelekeza.

"Asilimia 87.4 ya wajawazito sawa na akinamama 886,810 walipatiwa dawa za kukinga Malaria na jumla ya dozi 2,844,174 sawa na asilimia 84.6 walipewa dawa ya kuzuia upungufu wa damu(FEFOL),"amesema

Habari Kubwa