Wajawazito na watoto kupimwa ugonjwa wa kifua kikuu

10Apr 2017
Na Mwandishi Wetu
Dodoma
Nipashe
Wajawazito na watoto kupimwa ugonjwa wa kifua kikuu

ILI kukabiliana ugonjwa wa kifua kikuu nchni, serikali imeweka mpango kwa kila mama mjamzito na mtoto wa umri wa miaka chini ya mitano kupimwa ugonjwa huo na Ukimwi ili kupata takwimu sahihi.

Ummy Mwalimu.

Hayo yamesemwa leo Bungeni na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mbunge wa Busanda (CCM), Lolesia Bukwimba.

Bukwimba, alitaka kujua ni kwa jinsi gani serikali inafahamu tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu na kwamba unaathiri watu wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji wa madini na wale wanaoishi kandokando na maeneo ya wafugaji.

Akijubu swali hilo Mwalimu, amesema kuwa zaidi ya watu 100,000 wana ugonjwa wa kifua kikuu lakini wapo majumbani hawajafika katika vituo vya afya kupatiwa matibabu.

Amesema uwepo wa idadi hiyo majumbani ni jambo ambalo ni hatari kwa sababu wanatakiwa kupelekwa hospitalini kwa ajili ya kupata huduma.

“Mgonjwa mmoja wa kifua kikuu akiachwa bila ya kupata huduma ana uwezo wa kuwaambukiza watu 20 kwa mwaka,”amesema Mwalimu.

Habari Kubwa