Wajilipua kwa petroli kisa wazazi wa mwanaume kumkataa mwanamke

16Jun 2021
Marco Maduhu
SHINYANGA
Nipashe
Wajilipua kwa petroli kisa wazazi wa mwanaume kumkataa mwanamke

Wenslausi James (30), mkazi wa kijiji cha Busongo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, amejilipua moto pamoja na mke wake Betha Kasimili (25), kwa kutumia mafuta ya Petrol, kwa madai ya wazazi wake kumkataa mke wake.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga, Kamishina Msaidizi wa Polisi Jackson Mwakagonda.

Tukio hilo limetokea June 14 mwaka huu majira ya saa 4 asabuhi, katika kijiji cha Busongo Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu, nyumbani kwao na mwanamke.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga Kamishina msaidizi wa Polisi, Jackson Mwakagonda, akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.

Amesema wanandoa hao walikuwa wamezaa watoto watatu, lakini wazazi wa mwanaume walimkataa mkewake, na kuamua kuuvunja mji pamoja na kurudisha Mahali nyumbani kwao na mwanamke.

Habari Kubwa