Wakamatwa kwa tuhuma kujifanya maofisa ofisi ya Rais

04Jun 2021
Nebart Msokwa
Mbeya
Nipashe
Wakamatwa kwa tuhuma kujifanya maofisa ofisi ya Rais

WATU watano wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kujifanya maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na kuwatapeli wananchi fedha kwa njia ya mtandao kwa ahadi za kuwapatia ajira kwenye taasisi mbalimbali za umma.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni, Kessy Obere (24) Mkazi wa Kata ya Iwalanje katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.

Alisema kijana huyo ndiye alikuwa kinara wa kundi hilo na alikuwa anajitambulisha kuwa ni Waziri wa TAMISEMI na wakati mwingine amekuwa akijitambulisha kuwa yeye ni Mkuu wa Moja ya Wilaya za Mkoa wa Mbeya.

Alisema kijana huyo amekuwa akitumia laini mbalimbali za simu kuwatumia watu jumbe zinazoashiria kuwa kuna nafasi za ajira zimetangazwa na wanatakiwa kuziomba na yeye atawasaidia waajiriwe kwenye nafasi hizo.

Habari Kubwa