Hayo yalibainishwa jana na Naibu Waziri wa Maji, Maryprisca Mahundi wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza ambapo alitembelea mradi wa maji Sawa uliopo Nyamagana na mradi wa Buswelu Wilaya Ilemela.
Alisema lengo la ziara hiyo ni kuyafikia maeneo yenye miradi iliyosimama kwa muda mrefu ili kupata ufumbuzi ambao utasaidia upatikanaji wa maji kwa wananchi hivyo wakandarasi wazembe watakaochelewesha miradi wizara haitowavumilia bali itafatilia ukomo wa mkataba ambayo itaonyesha masharti na vigezo ambavyo watavizingatia pia miradi hiyo itaendelea kusimamiwa na wataalamu wa ndani kupitia Force akaunti ili kukamilisha.
"Hakuna kuongeza muda labda pawe pametokea tetemeko ,mafuriko yaliyosababisha kusombwa kwa miundombinu hayo tutayazingatia lakini kwa wale wasiokuwa na sababu hizo tutavunja hiyo mikataba" alisema Mahundi.
Alisema baada ya miaka mitano wananchi watapunguziwa adha ya maji ambapo upatikanaji wake kwa maeneo ya mijini itakuwa zaidi ya asilimia 95 huku vijijini ikiwa asilimia 85 hadi sasa hali inaridhisha kwani miradi mingi miundombinu imefanyika kilichobaki ni umaliziaji ili kufikia wiki ya maji mwezi March mwaka huu wanazindua ili kuhakikisha maji yanatoka bombani.