Wakazi Missenyi waaswa kutopuuza Corona

15Sep 2021
Lilian Lugakingira
BUKOBA
Nipashe
Wakazi Missenyi waaswa kutopuuza Corona

Wakazi wa Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera wametakiwa kutopuuza uwepo wa maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona, na badala yake waendelee kuchukua tahadhari zote za kujikinga.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa albam ya mwimbaji wa nyimbo za injili Maneno Mwandiga uliofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - KKKT- usharika wa Kyaka, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Projestus Tegamaisho ameshangaa katika mkusanyiko huo watu hawaoni umuhimu wa kutakasa mikono na wala hawajavaa barakoa.

"Ndugu zangu tusiufanyie mzaha ugonjwa huu maana nao hauna mzaha kwetu, tuendelee kujikinga kwa kufuata maelekezo tunayopewa na wataalamu wa afya ikiwamo kutakasa mikono kwa maji tiririka na sabuni lakini pia tuvae barakoa hasa tunapokuwa katika mikusanyiko" amesema  Tegamaisho.

Habari Kubwa