Wakazi wa Kisarawe kupata maji ya uhakika Septemba

11Jul 2019
Na Mwandishi Wetu
Kisarawe
Nipashe
Wakazi wa Kisarawe kupata maji ya uhakika Septemba

Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka Dar es salaam (DAWASA ) Jeneral mstaafu Davis Mwamunyange amekagua Maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa tenki la Kisarawe linalotarajiwa kukamilika Mwezi Septemba mwaka huu.

Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka Dar es salaam (DAWASA )Jeneral mstaafu Davis Mwamunyange akipewa maelezo ya Mradi wa tanki la Kisarawe kutoka kwa wataalamu.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo katika ziara hiyo Mwamunyange amesema kuwa lengo ni kukamilisha mradi kwa wakati kama ilivyo kwenye mkataba ili wananchi waweze kupata Huduma ya maji Safi.

“Mradi huu ambao ulianza rasmi mwaka jana unategemea kukamilika Septemba mwaka huu na utanufaisha wakazi wa Kisarawe, Ukonga pamoja na Pugu ambapo kutakuwa na upatikanaji wa maji ya uakika,”amesema

Aidha Mwamunyange amesema kuwa ipo miradi ambayo mpka sasa maendeleo yake ni mazuri na kuwataka wakandarasi waongeze juhudi ili wakamilishe kwa wakati.

“Mpaka sasa Maendeleo ya Mradi ni mazuri na nina amini mpaka mwezi Septemba mwaka huu ambayo wamesema utakua umesha malizika na Wanachi wa wilaya ya Kisarawe na vitongoji vyake watanufaika na mradi huu,”amesema Mwamunyange

Habari Kubwa