Wakili kortini kwa kughushi muhuri wa mahakama

23Sep 2016
Hellen Mwango
Nipashe
Wakili kortini kwa kughushi muhuri wa mahakama

WATU watatu akiwamo wakili wa kujitegemea, Godwin Muganyizi (44), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi na kujaribu kujipatia Sh. milioni 51.6 kutoka benki ya NMB.

Tanesco imeamriwa kulipa kiasi hicho wiki iliyopita katika hukumu ya mgogoro wake wa muda mrefu wa kisheria juu ya kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

Fedha zilizookolewa na Tanesco zinatokana na ukweli kuwa mwaka 2010 SCB-HK ilidai katika Baraza la Kimataifa la Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) jumla ya dola milioni 396.7 (zaidi ya Sh. bilioni 860) kutoka kwa shirika hilo la nishati.

Baraza la ICSID lenye makao yake jijini Washington DC, Marekani ni sehemu ya Benki ya Dunia na linagharimiwa na taasisi hiyo ya kimataifa ya fedha.

Kiasi cha fedha kilichookolewa kinaweza kuwa hata kikubwa zaidi kama Tanesco itadai kurejeshewa fedha kutoka kwa wamiliki wapya wa IPTL, kampuni ya Pan Africa Power Solutions (PAP), kwa sababu kwa kulipwa fedha zote za akaunti ya escrow, shirika la nishati la taifa lilipiga mahesabu yake katika viwango vya awali, ambavyo ilishavipinga katika baraza hilo la kimataifa kwa miaka kadhaa.

“Kwa hukumu ya hivi karibuni, hata PAP italazimika kurudisha kwa Tanesco kiasi kikubwa cha fedha ilicholipwa, kwa sababu fedha za escrow zililipwa kwa kutumia bei ya umeme ya zamani… Ndiyo sababu kwa kutazama (jambo hili) kisheria, Tanesco pia imepata ushindi mkubwa,” Richard Rweyongeza, wakili aliyeiwakilisha shirika hilo la umeme kwenye baraza hilo la kimataifa aliiambia Nipashe.

TANESCO IMESHINDA
Rweyongeza alikuwa akitoa tafsiri yake ya kisheria juu ya mgogoro huo uliofikia tamati Septemba 12.
“Kama utasoma hukumu kama inavyoonekana, inaweza kuonekana kuwa (shirika) limepoteza kila kitu, lakini nakuhakikishia, pande zote mbili zimeshinda na Tanesco imeshinda zaidi."

Kwa mujibu wa Rweyongeza, kama mahesabu ya ICSID yakifuatwa kikamilifu, hata kima cha tozo ya uwekezaji kinacholipwa kwa PAP kinaweza kupungua kwa karibu asilimia 50 mpaka kuwa Sh. bilioni 2.5 kwa mwezi.

Kwa sasa, shirika hilo limekuwa likilipa tozo ya uwekezaji kwa PAP inayofikia Sh. bilioni tano tangu Januari 2014.
“Ieleweke kuwa Tanesco ilikuwa ikipinga kiwango cha bei ya umeme kinachotozwa na IPTL, si kiasi cha mkopo kilichotolewa na benki za kigeni wakati wa ujenzi wa kituo cha kufua umeme cha Tegeta," alisema zaidi Rweyongeza kuiambia Nipashe.

"Sasa ukweli kuwa kiwango cha bei kimepunguzwa una matokeo makubwa kifedha ambayo yanakwenda mbali zaidi ya hukumu ya kulipa zaidi ya Sh. bilioni 320.

“Kwa kufanikiwa kupunguza kiasi cha hukumu kutoka pale kilipokuwa, kwetu ni mafanikio makubwa."
Kwa mujibu wa Rweyongeza, kama sakata la escrow lisingetokea, Tanesco ingepata ushindi wa asilimia 100 kwenye kesi hiyo, kwa sababu lalamiko lake kuu kwamba bei ya umeme inayotozwa na IPTL ni kubwa lilikubaliwa na baraza hilo la usuluhishi la kimataifa.

Uamuzi huo wa ICSID umekuja miaka mitatu tangu serikali iruhusu kitatanishi kufanyika kwa malipo ya dola milioni 200 (sawa na Sh. bilioni 440) kutoka katika akaunti ya Tegeta escrow kwenda kwa kampuni ya Harbinder Singh Sethi ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited(PAP).

Agosti 2005, SCB-HK ilinunua kwa bei ya punguzo ya dola za Marekani 76.1 kutoka benki ya Malaysia ya Danaharta, baada ya benki hiyo kushindwa kurejesha deni lake la muda mrefu kutoka IPTL.

Bei halisi ya deni hilo ilikuwa dola milioni 101.7, kwa mujibu wa ushahidi uliopo. IPTL ilikopa zaidi ya dola milioni 100 mwaka 1998 kutoka kwa ubia wa mabenki ya Malaysia ili kujenga mtambo wa kufua umeme wa megawati 100 wa Tegeta.

Habari Kubwa