Wakulima wa korosho walipwa bil. 133/-

17Dec 2018
Na Mwandishi Wetu
Mtwara
Nipashe
Wakulima wa korosho walipwa bil. 133/-

WAKULIMA wa korosho wamelipwa jumla ya Sh. 133,259,933.855, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema.

wakulima wa korosho.

Waziri Hasunga amesema kwamba fedha hizo zililipwa kwa wakulima hao hadi kufikia Jumamosi.

Hasunga alitoa takwimu hizo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa wabanguaji uliofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.

Alisema kuwa katika Mkoa wa Mtwara wananchi ambao wamekwishalipwa ni 77,055, huku jumla ya fedha iliyolipwa ni Sh. 80,098,982,060.

Katika mkoa wa Lindi tayari wakulima 41,564 wamekwishalipwa kiasi cha Sh. 42,502,635,227, huku katika mkoa wa Ruvuma wakulima 11,463 wamekwishalipwa kiasi cha Sh. 10,557,222,943.

Aidha, Hasunga amesema kuwa katika mkoa wa Pwani Sh. 101,091,960 zimekwishalipwa kwa wakulima 81.

Aidha, vyama vilivyohakikiwa ni 461 na vilivyolipwa ni 451.

Habari Kubwa