Wakwama kwenda shule kisa umbali

07Dec 2021
Julieth Mkireri
Kibaha
Nipashe
Wakwama kwenda shule kisa umbali

WANAFUNZI 50 wa Kata ya Boko Mnemela katika Wilaya ya Kibaha wameshindwa kuanza masomo ya sekondari kutokana na kushindwa kutembea umbali wa kilomita tisa.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Elimu wa Kata hiyo, Haiba Sanze, alipokuwa akitoa taarifa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Shule ya Sekondari katika Kata ya Boko Mnemela iliyoandaliwa na Mbunge na Mbunge wa Kibaha Vijijini, Michael Mwakamo.

Alisema idadi hiyo ni kwa miaka mitatu mfululizo ambapo pia mbali ya wanafunzi hao kushindwa kuanza kidato cha kwanza, wapo zaidi ya 20 wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na kikwazo hicho cha umbali na wazazi kushindwa kumudu kuwalipia nauli ya bodaboda kila siku. 

Kutokana na hali hiyo Mbunge Mwakamo amefanya harambee kuchangia tofali na mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari kunusuru wanafunzi wanaokosa elimu ya sekondari.

Habari Kubwa