Walemavu 51 wapatiwa msaada miguu bandia

21Feb 2021
Dotto Lameck
Iringa
Nipashe
Walemavu 51 wapatiwa msaada miguu bandia

KAMPUNI ya Kamal Group ya Jijini Dar es Salaam imetoa miguu bandia kwa watu 51 wenye ulemavu wa viungo ambapo imepelekea kurejesha furaha ambayo hawakutarajia kutokana na gharama kubwa za viungo hivyo bandia.

Stela Nyaki.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo kwa wahusika na mbele ya Mbunge wa viti maalumu, Ritta Kabati, Mratibu wa kampuni hiyo, Stela Nyaki, amesema kampuni hiyo inaamini kuwa inao wajibu wa kusaidia maendeleo katika jamii inayowazunguka.

“Tunaamini kuwa ni wajibu wetu kusaidia jamii inayotuzunguka ni wajibu wetu kuleta tabasamu katika nyuso za watu wanaotuzunguka na kuhakikisha kuwa wale wenye ulemavu wa miguu wanaweza kutembea tena,” amesema Nyaki.

Pia, Nyaki amesema lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanarudi katika sehemu zao za kazi ili watoe michango yao katika kuijenga Tanzania. Kwa vile tunacho kiwanda chenye zana za kimataifa hapa hapa nchini Tanzania.

Kwa upande wa baadhi ya walemavu waliopatiwa miguu hiyo wamemshukuru Mbunge Ritta Kabati, na kampuni hiyo kwa moyo wa pekee wa kuwajali wananchi wake kwa kuzingatia makundi yote kwenye jamii ambapo wamesema kwa sasa wataenda kufanya kazi na kuachana na utegemezi.

 

Habari Kubwa