Walimu sikio la kufa kushiriki mapenzi na wanafunzi

10Dec 2019
Shaban Njia
KAHAMA
Nipashe
Walimu sikio la kufa kushiriki mapenzi na wanafunzi

SERIKALI wilayani Kahama Mkoani Shinyanga imesema kuwa, wapo baadhi ya walimu wa Shule za Msingi na Sekondari ambao sio wahadilifu wamekuwa wakijihusisha kwenye vitendo vya mapenzi na wanafunzi wa shule hizo.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha.

Hayo yalibainisha leo Disemba 10, 2019 na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha wakati wa Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ambapo kiwilaya yamefanyika katika viwanja vya Bwalo la Polisi.

"Tumeshaanza kuwachukulia hatua za kisheria walimu wenye tabia za kutembea kimapenzi na wanafunzi....walimu msiokuwa na tabia za namna hiyo msikubali kuchafuliwa na baadhi ya walimu ambao sio wahadilifu, toeni taarifa ili tuwawajibishe kisheria" amesema Macha

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha.

Habari Kubwa