Walimu wanaofanya siasa, wamchefua DC Sabaya

28Feb 2019
Godfrey Mushi
Hai
Nipashe
Walimu wanaofanya siasa, wamchefua DC Sabaya

WALIMU wanaofanya siasa katika Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro ambazo zinaihujumu serikali ‘wamemchefua’ Mkuu wa Wilaya hiyo Lengai Ole Sabaya na kulazimika kutoa onyo kali, akitaka wawaachie shughuli hiyo wanasiasa na Chama cha Mapinduzi (CCM) watekeleze ilani yake ya uchaguzi hadi mwaka 2020.

Mkuu wa Wilaya hai, Lengai Ole Sabaya.

“Mkurugenzi (Yohana Sintoo), naomba uwaonye watumishi hawa, muache, muache kufanya siasa zinazoihujumu serikali. Muache kufanya siasa, waacheni wanasiasa, waacheni CCM watekeleze ilani yao kwa kishindo hadi mwaka 2020, lakini si kwa sababu mwalimu mmoja ameamua kuwasaidia watu wengine,”alionya

Sabaya ametoa onyo hilo Leo Februari 28,2019 wakati alipokutana na walimu wakuu wa shule za msingi, sekondari, waratibu wa elimu kata, watendaji wa vijiji, kata na maafisa elimu katika kikao kazi cha siku moja kutoa maelekezo yake kwenye sekta ya elimu.

Aidha katika kikao kazi hicho, Sabaya amewatahadharisha walimu hao, kamwe wasijaribu kutengua kwa namna yeyote ile maelekezo ya Rais Dk. John Magufuli kuhusu uchangishaji wa michango katika shule za msingi na sekondari.

“Msitengue kwa namna yeyote maelekezo ya mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Suala la michango mashuleni msijuhusishe nalo, waacheni wazazi na kamati zao wafanye maamuzi husika, lakini katika kukusanya michango hiyo, ninyi hamtashiriki,"Amesema Sabaya na kuongeza;

"Melekezo kuhusu chakula cha mchana, sasa mimi nataka tuelewane, mwanafunzi akiwa nyumbani si anakula, chakula ni basic needs (hitaji muhimu) na siyo ethically reguirement (hitaji la kimaadili),”ameeleza Sabaya

Habari Kubwa