Walimu wasikaimishwe nafasi za utendaji vijiji, mitaa na kata

16Sep 2021
Na Mwandishi Wetu
Pwani
Nipashe
Walimu wasikaimishwe nafasi za utendaji vijiji, mitaa na kata

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ummy Mwalimu, ametoa maelekezo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutowatumia walimu kukaimu nafasi za utendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata bali waachwe wafanye kazi yao ya kufundisha hasa kutokana na upungufu wa walimu uliopo hapa nc

Akiongea na Sekretarieti ya Mkoa wa Pwani Waziri Ummy amesema, Wakurugenzi wamekuwa wakiwatumia walimu kukaimu nafasi mbalimbali za utendaji na suala hilo halikubaliki kwa kuwa mwalimu ameajiriwa kwa lengo mahususi la kufundisha na sio kufanyakazi za kiutendaji.

“Kunachangamoto ya uhaba wa walimu nchini,hivyo tuwaache walimu wafanye kazi ya kufundisha, kwa kuwa jukumu kubwa la waalimu ni kufundisha wasikaimishwe kwenye utendaji wa kata, mitaa na vijiji” amesema Waziri Ummy

Waziri Ummy amesema kuwa Serikali inatambua ipo changamoto ya uhaba wa watendaji wa kata, vijiji na mitaa lakini amewataka Wakurugenzi kuanza kuwatumia watumishi wengine wa kada nyingine wakiwemo, maafisa maendeleo ya jamii ili kupunguza changamoto hiyo.