Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga, kupitia taarifa yake aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, alisema mwezi huu amepokea majalada mbalimbali kutoka vyombo vya upelelezi kwa ajili ya kuyapitia na kufanya uamuzi wa kufungua au kutofungua mashtaka likiwamo sakata hilo.
Alitaja mashtaka mengine yatakayowakabili watuhumiwa hao kuwa ni kujihusisha na uhalifu wa kupangwa kinyume cha Sheria ya Kuzuia Makosa ya Uhujumu Uchumi na Uhalifu wa Kupangwa Sura ya 200 marejeo ya mwaka 2019.
“Mashtaka mengine ni usafirishaji haramu wa binadamu kinyume cha Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu Na. 6 sita ya mwaka 2008, kushindwa kulipa kodi, ambapo katika nyumba ya kulala wageni ya Madiba ilibainika haikuwa na leseni na hivyo kukwepa kodi kinyume na Sheria ya Usimamizi wa Kodi sura ya 438 marejeo ya mwaka 2019,” alisema.
Soma zaidi: https:epaper.ippmedia.com