Walipwa mshahara wa matofali badala ya pesa

23Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Walipwa mshahara wa matofali badala ya pesa

Wafanyakazi katika kiwanda cha matofali kusini mashariki mwa China wanaokidai kiwanda hicho mishahara yao yenye thamani ya $14,050, sawa na TSH 300,000 wamelipwa matofali, inaripotiwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari Xinhua, takriban wafanyakazi 30 wa kiwanda hicho huko Nanchang, katika jimbo la Jiangxi , walikubali kulipwa matofali 290,000 badala ya mshahara wanaodai.

Matofali

Gazeti la Jiangxi Daily linaripoti kuwa wafanyakazi hao , wote wakiwa ni wahamiaji , wametoka katika eneo la milima la jimbo la Yunnan kuini magharibi, na hawakuwa na namna ili kuishi kwa "kutumia mishumaa na kuwasha kuni moto ili kupunguza baridi ".

Chanzo: BBC  

Habari Kubwa