Wamiliki wa Baa kuchangamkia fursa ya SBL ‘Raise the Bar’

20Jul 2021
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wamiliki wa Baa kuchangamkia fursa ya SBL ‘Raise the Bar’

Baada ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kutangaza mpango wake maalum wa kusaidia baa kupambana na magonjwa ya kuambikiza ukiwamo ugonjwa wa corona, wamiliki wa baa wameanza kuchangamkia fursa hiyo kwa kujisajili kwenye mpango huo.

Msaada huo una thamani ya shilingi bilioni 2.3 ni mahsusi  kwa ajili ya kulinda afya za wateja pamoja na wahudumu. Msaada huu wa SBL unakuja wakati dunia ikikumbwa na wimbi la tatu la ugonjwa wa corona huku nchi mbalimbali zikipambana kuwakinga raia wake ili kuhakikisha shughuli za kiuchumi zinaendelea kama kawaida.

Programu hii inayojulikana kama “Raise the Bar” au “Tunyanyuke Pamoja”, itadumu kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwezi huu Julai 2021 na baa zitapata misaada ya vifaa na mafunzo baada ya kujiandikisha na kukidhi vigezo maalumu.

Mwakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, Faith Mpawa, (kulia) akimuelekeza mmoja wa wafanyakazi wa baa ya Meridian iliyopo Vijana Kinondoni namna ya kujisajili katika Mpango wa kuzisaidia baa kunyanyuka maarufu kama Raise the Bar unaofadhiliwa na Kampuni hiyo.
Hassan Matata (kulia) akimwelekeza mmoja wa wafanyakazi wa MK bar iliyopo jijini Dar es Salaam namna ya kujaza fomu ya maombi kwa ajili ya kuomba misaada mbali mbali inayotolewa na Kampuni ya SBL kupitia mpango wa kusaidia baa kunyanyuka maarufu kama Raise the Bar.
Mwakilishi wa kampuni ya Bia ya Serengeti alimwelekeza mmoja wa wateja namna ambavyo anaweza kujaza fomu kwa ajili ya kuomba kunufaika na mradi wa kunyanyua baa baada ya kuathiriwa na ugonjwa wa corona unaojulikana kama Raise the Bar.
Mmoja kati ya wateja waliofika katika banda lililowekwa kwa ajili ya kuwaelekeza wenye mabaa namna ya kujisajili katika mpango wa kuyasaidia mabaa kunyanyuka unaojulikana kama Raise the Bar au Tunyanyuke Pamoja akipata maelekezo kutoka kwa wawakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti.