Wamwangukia Lukuvi kupata kibali cha ujenzi

08Apr 2021
Peter Mkwavila
Dodoma
Nipashe
Wamwangukia Lukuvi kupata kibali cha ujenzi

WAKAZI wa mtaa wa Mtakuja mji Mwema kata ya Chang’ombe jiji la Dodoma amemuomba Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo na Makazi Wiliam Lukuvi, kutoa kibali cha ujenzi wa nyumba kwenye maeneo yao ili waweze kuondokana na maisha duni ya kukosa makazi bora.

Ombi hilo kwa Waziri lilitolewa na wakazi hao kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mji mwema, ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya kumuomba waziri wa ardhi ili aweze kutoa kibali kitakacho wawezesha kujenga makazi bora tufauti na wanavyoishi kwa hivi sasa.

Waziri Lukuvi alisimamisha ujenzi wa nyumba kwenye mtaa huo wa Mji Mwema kata ya Chang’ombe jijini Dodoma, Julai15 2020, kwa madai kuwa kampuni iliyopima ya J.F. kwenye mtaa huo wa Mtakuja Mji Mwema ilikuwa haitambuliwi kisheria na serikali na imefutwa.

Wakizungumza kwenye mkutano huo wakazi hao, Daniel Kiula, amessema kuwa toka walivyosimamishwa kuendeleza maeneo yao, maisha yao yamekuwa ni duni kwa kuwa walio wengi pamoja na kuwa wana hati lakini wanashindwa kokopea fedha ili waweze kujenga nyumba za kisasa.

Pili Sukuma, amesema wanamuomba waziri huyo mwenye dhamana kuwatatulia changamoto hiyo iliyojitokeza ya kuzuuliwa kujenga nyumba kwenye maeneo hayo,ili aweze kutoa kibari ambacho yeye aliamuru kuisimamisha kampuni hiyo ilikuwa ikipima na ambayo ilidaiwa kuwa haitambuliwi kisheria na serikali.

“Tunamuomba waziri wetu Lukuvi awe na jicho la huruma aje atengue kifungo hichi tulichofungwa cha kuzuuliwa kujenga kwenye maeneo yetu ambayo hata hivyo tayari yameshapimwa,wengi wetu hapa tumna hati na vibari vya kujenga ili tuondokana na hizi nyumba ambazo ni duni kwa maisha ya mtanzania” amesema.

Habari Kubwa