Wanachama 10 UWT wasimamishwa uanachama kisa rushwa

09Jul 2020
Marco Maduhu
SHINYANGA
Nipashe
Wanachama 10 UWT wasimamishwa uanachama kisa rushwa

Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Said Bwanga, ametaja majina ya viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT, pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa, Asha Makwaiya, kusimamishwa uanachama baada ya kutuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Katibu wa siasa na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga.

Ametaja majina hayo leo mbele ya waandishi wa habari kuwa ni Hulda Malsaba, Pendo Mhapa, Zulfa Hassani, Jackline Isalo, Elizabeth Hange, Moshi Ndugulile, Tabu Shabani, Happy Chikala, Elzabeth Buzwizwi, pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa Asha Makwaiya.

Katika hatua nyingine Bwanga amesema kuwa chama hicho kimetangaza majina ya wanachama 10 waliotia nia ya kugombea kupitishwa kugombea Ubunge Shinyanga Mjini.

"Hadi leo asubuhi Alhamis Julai 9,2020 jumla ya wanachama wa CCM 10 wamejitokeza kutia nia kugombea kiti cha Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini na zoezi la kuchukua fomu kugombea ubunge litafanyika Julai 14,2020 hadi Julai 17,2020"

Bwanga, amewataja waliojitokeza kutia nia ya kuwania Ubunge Shinyanga Mjini kuwa ni Stephen Julius Masele, Dotto Joshua, Erasto Kwilasa, Bandora Salum Mrambo, Wilbert Masanja, Severine Luhende Kilulya, Jonathan Manyama, Lydia Winga Pius, Mary Izengo na Eunice Jackson.

 

Habari Kubwa