Wanachama 30 Shinyanga wajitokeza kuchukua fomu ubunge

14Jul 2020
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe
Wanachama 30 Shinyanga wajitokeza kuchukua fomu ubunge

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnea Bashemu akitaja majina ya wagombea Ubunge Shinyanga mjini ambao Leo wamechukua fomu, kuwa wamefika 30, wanaume 24, wanawake Sita.

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnea Bashemu.

Mmoja wa aliyejitokeza ni Stephen Masele anayetetea kiti chake kwa mara ya tatu, akifuatiwa na Dotto Joshua, Hassani Fatiu, Mussa Ngangala, Benjamini Chagula, Bandora Mirambo,Ramadhani Ramadhani, Austin Makani, Stanley  Mayunga, John Mlyambate, Severine Kilulya, Kulwa Meshack, Francis Kasili.

Wengine ni Paulo Nangi, Gratian Rwekaz, Leonard Mapolu, Godfrey Msemakweli, Wilbeth Masanja, John Makune, Erasto Kwilasa, Yohan Mapesa, Jonathan Ifunda, Gasper Kileo na Joab Kaijage.

Kwa upande wa wanawake waliochukua fomu ya kugombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini ni Grace Lyon, Eunice Wisha, Veronica Mirambo, Hamisa Magulu, Lyidia Pius pamoja na Mary Izengo.

Habari Kubwa