Kikundi cha Maarifa Women Group kilichopo mtaa wa Manzese na Mavuno kilichopo mtaa wa Mvuleni, vimetoa msaada huo mwishoni wa wiki baada kukusanya jumla ya Sh. 700,000.
Mwanzilishi wa vikundi hivyo Mwalimu Wenclaus Mutatina akizungumza baada ya kutoa vifaa hivyo kwa watoto waishio mitaa hiyo, amesema vikundi hivyo vinavyoundwa na wazazi, walezi wamechangishana fedha na kununua madaftari na kalamu kusaidia wazazi wa mtaa wa Kilimani, ambao hawana uwezo wa kumudu gharama ununuzi vifaa hivyo.