Wananchi wametakiwa kutowanyanyapaa watu wenye ulemavu

15Sep 2021
Marco Maduhu
Dar es Salaam
Nipashe
Wananchi wametakiwa kutowanyanyapaa watu wenye ulemavu

MKE wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Zainab Shaib, amewataka Wananchi kutowanyanya paa watu wenye ulemavu, pamoja na Serikali kuwawezesha mikopo ya asilimia 2, ili wajikwamue kiuchumi.

Shaibu alibainisha hayo hivi karibuni, kwenye mkutano wa waandishi wa habari na wahariri, uliofanyika kwa njia ya mtandao Zoom, ulioandaliwa na Shirika la Internews.

Alisema watu wenye ulemavu ni sawa na watu wengine, ambapo wanauwezo wa kufanya kazi endapo wakiwezeshwa, na hivyo kuwataka wananchi wasiwabague, bali washilikiane nao kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi.

"Naomba waandishi wa habari, muendele kuandika habari za watu wenye ulemavu, na kuonyesha mambo ambayo wanayafanya ya shughuli zao za kiuchumi ili kuonyesha jamii kuwa wanaweza," alisema Shaibu."

Pia Halmashauri ziendelee kiwapatia fedha za mikopo  asilimia 2 watu wenye ulemavu ,ili wazitumie kuanzisha shughulia za kuwaingizia kipato na kuinuka kiuchumi," aliongeza.

Naye Mhairiri mtendaji wa Gazeti la Nipashe Beatrice Bandawe, alisema waandishi wa habari wamefanya kazi kubwa ya kuandika habari za watu wenye ulemavu, ambapo wamesaidia kutatua baadhi ya changamoto, wakiwamo watoto waliofichwa ndani kupata ufadhili wa masomo.

Kwa upande wake Mkuu wa Kanda wa miradi kutoka Shirika hilo la Internews Jackie Lidubwi,  awali akifungua mkutano huo, alisema vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa sana kupaza sauti za watu wenye ulemavu na kutatuliwa matatizo yao.

Habari Kubwa