Wananchi waomba matembezi ya hiyari kumpongeza Rais

23Jun 2022
Neema Hussein
Katavi
Nipashe
Wananchi waomba matembezi ya hiyari kumpongeza Rais

Wananchi mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wakulima, wajasiriamali, wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya Mkoa wa Katavi pamoja na watumishi wa taasisi za serikali na binafsi wameiomba ofisi ya mkuu wa Mkoa kufanya matembezi ya hiyari kuipongeza serikali ya awamu ya sita.

Maombi hayo yametokana na wananchi hao kuguswa na utendaji mzuri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kutokana na mambo makubwa ambayo Rais ameyafanya katika kipindi cha uongozi wake.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema kama serikali wanaheshimu hisia na matakwa ya wananchi wake hivyo wanaungana na wananchi katika kutelekeza adhma hiyo njema ya kufanya matembezi ya hiyari ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Matembezi hayo ya hiyari yanatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya tarehe 25 Juni 2022 na yataanza mapema saa 12:30 asubuhi katika uwanja wa Polisi Buzogwe na kelekea uwanja wa Kashaulili ambako matembezi hayo yatapokelewa rasmi.

Habari Kubwa