Wanaojikojolea kitandani waitwa kupata matibabu

29Aug 2021
Rahma Suleiman
ZANZIBAR
Nipashe Jumapili
Wanaojikojolea kitandani waitwa kupata matibabu

DAKTARI wa magonjwa ya akili katika Hospital ya Kidongochengundu Visiwani Zanzibar, Khadija Abdulrahman Omar, amewataka wananchi wenye tatizo la kukojoa kitandani (vikojozi) kutoona aibu kwenda hospitalini hapo kufuata matibabu kwa sababu huo ni ugonjwa.

daktari Khadija Abdulrahman Omar.

Akizungumza na Nipashe ofisini kwake Kidongochekundu Mjini Zanzibar, amesema tatizo hilo ni maradhi kama yalivyo maradhi mengine hivyo ni vyema kufuata tiba haraka.

Amesema mtu aliefikia umri wa miaka sita na kuendelea ambae anakojoa kitandani anatatizo la kiafya na anahitaji kupata tiba haraka.

Amesema tatizo hilo lipo lakini watu wengi wanaona aibu kufuata huduma za matibabu hospitalini kutokana na kunyanyapaliwa katika familia zao.