Wanawake CCM,Chadema jino kwa jino siku ya wanawake duniani

08Mar 2019
Na Mwandishi Wetu
GEITA
Nipashe
Wanawake CCM,Chadema jino kwa jino siku ya wanawake duniani

Baada ya Polisi wilayani Geita limekizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuadhimisha siku ya wanawake duniani,wanawake wa vyama vya Chadema waliamua kuwafuata wa CCM huku wakinyoosheana vidole vya ishara ya vyama vyao.

Hiyo ni baada ya baadhi ya wakereketwa na viongozi wa Umoja wa wanawake(UWT) Mkoa wa Geita kuonyeshwa kukerwa na hatua ya wanawake wa CHADEMA kujumuika pamoja nao kwenye viwanja vya soko jipya kata ya Kalangalala kama walivyoamuliwa na Jeshi la polisi.

Kutokana na hali hiyo,wanawake na wanachama wa CHADEMA na viongozi mbalimbali wa kitaifa waliokwishawasili mkoani humo, walilazimika kuungana na wenzao kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kusherehekea siku hiyo jambo lililozua minong’ono ya hapa na pale kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa CCM na kuvilazimu vyombo vya ulinzi na usalama kuwa na wakati mgumu kuwatuliza.

Chadema wameonekana wakiwa wamekaa katika maeneo yao wakiwa na sare zao huku kina mama wa CCM nao wakiwa na sare za chama chao katika viwanja vya soko jipya mjini Geita.

 

Katika barua iliyotolewa na mkuu wa polisi wilaya, Ally Kitumbu iliyotolewa jana Alhamisi Machi 7, 2019 kwa katibu wa Chadema Geita yenye kumbukumbu namba GE/B.3/24/VOL.V11/63 imewataka wanawake kushiriki maadhimisho hayo maeneo ya Bugulula halmashauri ya wilaya na viwanja vya soko jipya yanakoadhimishwa na halmashauri ya mji.

Habari Kubwa