Wanawake Hanang' waacha ukeketaji

22Oct 2021
Cynthia Mwilolezi
Hanang'
Nipashe
Wanawake Hanang' waacha ukeketaji

WANAWAKE waliokuwa wakijishughulisha na kazi ya ukeketaji wa jamii ya watadoga na wanyaturu kwenye Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara, wameamua kuacha kazi hiyo na kujishughulisha na ujasiriamali.

Ngariba hao wameamua kujikita kwenye  ujasiriamali  na kufanya shughuli za utunzaji wa ng’ombe wa maziwa, ufugaji nyuki na kuachana na ukeketaji waliokuwa wanawafanyia wasichana.

Akizungumza leo wilayani  Hanang' na Nipashe mmoja wa wanawake hao,walisema wameingia  kwenye  ufugaji nyuki na utunzaji wa ng’ombe wa maziwa, vinavyofadhiliwa na Shirika la Oxfam na kuratibiwa na Shirika la Ujamaa la UCRT.

Pascalina Michael amesema mbali na vita inayopigwa na  serikali juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia lakini vinaendelea wameona bora waachane na kazi hiyo na kujikita na kazi zingine.

"Serikali  inapiga vita ukeketaji wa mabinti kila siku  tunaendelea mimi na wemzangu tumeona tufanye kazi zingine  na tunaomba wanaoendelea kufanya kazi hii tena kwa watoto wadogo waache waje kwenye  ujasiriamali,"alsiema na kuongeza:

“Suala la kupiga  vita dhidi ya ukatili wa kijinsia na unyanyapaa imekuwa mkombozi kwetu wanawake lakini tunaiomba Serikali ielekeze nguvu hii katika kuwakagua watoto wanapokwenda kutibiwa au kliniki kwani vitendo vya ukeketaji vinafanywa na sasa ni kwa watoto wachanga si kwa wakubwa tena,” amesema.

Tatu Abdalah amesema yeye awali alikuwa anaishi Singida na kuhamia wilayani Hanang ambapo alikuwa anajihusisha na ukeketaji wa wasichana wa maeneo hayo.

Tatu amesema kutokana na miangaiko yake na vikwazo vya serikali ameamua kuachana na matukio ya ukeketaji na kujishughulisha na ujasiriamali ili ajiingizie kipato.

“Mangariba wengi wanafanya kazi ya kukeketa watoto wa watu kwa sababu ya kupata kipato ila kwa sababu hivi sasa serikali imeingilia hili jambo kwa nguvu kubwa tumeamua kutupa nyembe chini,” amesema Tatu.

Ofisa wa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Hanang’, Sarah Erasto amesema vita vya ukatili wa kijinsia kwa mwanamke vinaanza kwa wanawake wenyewe.

Habari Kubwa