Wanawake kuwezeshwa kiuchumi kujikinga na udhalilishaji

16Jan 2019
Rahma Suleiman
ZANZIBAR
Nipashe
Wanawake kuwezeshwa kiuchumi kujikinga na udhalilishaji

Chama cha Waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa upande wa Zanzibar imesema kuwa wamekuwa wakiwawezesha wanawake kiuchumi ili kuwakinga na vitendo vya udhalilishaji. 

Asha Abdi wa kwanza kulia akizungumza katika kikao na kamati ya maendeleo, habari, utalii na wanawake ya baraza la wawakilishi katika Ofisi za Tamwa Tunguu Zanzibar

Akizungumza na kamati ya maendeleo ya wanawake, habari, utalii na maendeleo ya baraza la wawakilishi Asha Abdi Ofisa kutoka Tamwa, amesema kuwa wanawake waliowawezesha kiuchumi wameongeza mapenzi kwa waume zao. 

"Wanaume wanapowaona wake zao wanafanya biashara na fedha wanazopata wanasaidia familia mapenzi yameongezeka katika ndoa zao"alisema Asha Abdi.

Amesema hali hiyo imesaidia wanawake kutodhalilishwa katika ndoa na kuondokana na utegemezi kutoka kwa waume zao .

 

Habari Kubwa