Wanawake vyama vya siasa wadai kufanyiwa ukatili kugombea uongozi

25Nov 2021
Yasmine Protace
Nipashe
Wanawake vyama vya siasa wadai kufanyiwa ukatili kugombea uongozi

KATIKA kuelekea  siku 16 za kupinga ukatili duniani kote, wanawake ambao ni viongozi  kutoka vyama 19 vya siasa hapa nchini, wamedai baadhi ya vyama vyao vimekuwa vikiwafanyia ukatili wa kijinsia wanawake katika kugombea nafasi za juu za uongozi.

Mbali na ukatili wa kijinsia pia baadhi ya vyama vyao vimekuwa vikiwafanyia ukatili wa kiuchumi wanawake hao kwa kutowapatia fedha za ziara za chama na kuwataka wajihudumie wenyewe.

Viongozi hao baadhi yao wamedai  kutokana na kuwa na idadi ndogo ya wanawake katika vikao vya ngazi za juu hali hiyo imechangia kushindwa kushiriki katika vikao vya maamuzi.

Katika warsha ya siku tatu iliyoandakiwa na TGNP Mtandao, iliwashirikisha viongozi wanawake na vijana wa kike.

Warsha hiyo ukizungumzia umuhimu wa utekelezaji wa masuala ya kijinsia katika vyama vyao.Baadhi ya viongozi hao waliweza kuzungumzia utekelezaji wa masuala ya kijinsia katika vyama vyao.Pia viongozi hao waliweza kuzungumzia changamoto  wanazokutana nazo   katika vyama vyao.

Pia viongozi hao wameangalia masuala ya katiba za vyama zao yalivyoingiza masuala ya wanawake.Lengo lao ni kuhakikisha Kama katiba inaposema binadamu wote ni sawa,wao wanaona usawa haupo kutokana na nafasi za juu za uongozi bado zinashikiliwa na wanaume.

Mkurugenzi wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi amesema wapo wakitafari juu ya uwakilishi wa wanawake katika ngazi ya uongozi bado haijafikiwa.

Amesema   katika wanawake inatakiwa  uinatakiwa viongozi wawakilishi lazima uwe kwa asilimia 50.

Anasema sera za vyama vyote vimeingiza sera,lakini ukidodosa unaona changamoto.Anasema Ilan zinasema asilimia 50 kwa 50   lakini magepu yapo wazi.

Anasema kunapokuwa  na mchanganyiko wanawake na wanaume kuna kuwa na tija.

"Lakini wakiwa wanaume pekee  idadi kubwa  ya masuala ya kijinsia yanakuwa hayapo", amesema 

Anaongeza kuwa  masuala ya kijinsia yameingizwa vyama vyao kwa asilimia ngapi.

Anasema  ni kufanya  uchambuzi wa kina  kuona Kama masuala ya kijinsia yametekelezwa..

Anaongeza kuwa matarajio yao ni kuona vyama vya siasa vinatekeleza masuala ya kisiasa.

Grace Haule, ambaye ni Katibu wa (UWT) Mkoa wa Dar es Salaam anasema kuwa,kupitia mfumo wa vyama vingi, wanawake wa CCM wameweza  kupata haki katika chaguzi.

Habari Kubwa