Wapinzani wanaohamia CCM wapingwa mkutano mkuu

10Jul 2020
Enock Charles
DAR ES SALAAM
Nipashe
Wapinzani wanaohamia CCM wapingwa mkutano mkuu

WANACHAMA kutoka vyama vya Upinzani wanaohamia katika Chama cha Mapinduzi (CCM) wameelezwa kuchukua nafasi za waliokipigania chama hicho na kupewa nafasi mbalimbali za uongozi huku waliokipigania chama hicho wakiachwa.

Nsojo.

Akizungumza Jijini Dodoma leo mmoja ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho aliyejitambulisha kwa jina la Nsojo kutoka Mkoa wa Songwe amemueleza Mwenyekiti wa chama hicho Rais John Magufuli kuwa wanachama hao wamekuwa wakiwavunja moyo wenyeji kwa vile hupewa nafasi za kushika uongozi kwa haraka kuliko wanachama aliodai kuwa wamepigana kukitetea chama hicho.

“Kuna malalamiko ya wana Songwe kwamba wanachama wa vyama vya upinzani wanapotoka kule kuja kwetu ,kwetu ni neema na kama Katiba ya Chama cha Mapinduzi  inavyosema binadamu wote ni  sawa ni kweli tunawapokea lakini wananchi wamekuwa wakivunjika sana mioyo wanapopewa nafasi za uongozi “ amesema Nsojo.

“Wanapita wakiwaacha wanachama wa chama cha mapinduzi ambao walipigana kwa kufa na kupona kuanzia 2010 mpaka 2015  wengine kuchukuliwa hata mali zao wanavunjika moyo baada ya kuona wao wanapita bila mbadala” ameongeza

Akijibu hoja hiyo Rais Magufuli amesema kuwa katika chama hicho wanachama wote ni sawa na kuwataka wanachama wa chama hicho kutoweka mipaka ya kuzuia wanachama kuingia katika chama hicho na kuwapa nafasi watu wote kwa kuzingatia kuwa wanafuata misingi ya chama hicho bila upendeleo

“Nilifikiri hilo ungelizungumzia huko huko kwenye kamati ya siasa ya Wilaya na ya mkoa kwamba wanaokuja kule huwahitaji wewe lakini chama hiki ni chama cha watu kina misingi yake kina meza watu wote”

“Kwa hio mimi ningependa huyo aliyeingia aendelee kushinda tu siku moja hata awe mjumbe wa NEC (halmashauri kuu) kwani mke wako akikosea au mme wako akaja kuomba msamaha utakataa? Saa nyingine akaja na mapenzi mazuri mazuri kuliko ya zamani amejifunza huko mbinu nyingi na mbinu mbadala” amesema Rais Magufuli.

Habari Kubwa