Waratibu wa uchaguzi watakiwa kusoma sheria

03Aug 2020
Neema Emmanuel
MWANZA
Nipashe
Waratibu wa uchaguzi watakiwa kusoma sheria

Waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi,maofisa ugavi na maofisa uchaguzi kutoka Mkoa ya Mwanza na Mara watakiwa kusoma sheria za uchaguzi, kanuni na maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na tume.

Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Thomas Mihayo.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo ya siku tatu ya Watendaji wa uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28, mwaka huu Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Thomas Mihayo amesema njia hiyo itawasaidia kuwaongoza wakati wa utoaji wa mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi ngazi ya kata na vituo vya kupiga kura.

"Jukumu lililoko mbele yenu ni kutoa mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata ,kuteua makarani waongozaji wapiga kura,wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo katika uteuzi wa watendaji hao mnasisitizwa kuzingatia sifa, uadilifu na weledi wa waombaji wa nafasi hizo bila kupendelea ndugu au marafiki ambao watapelekea kuharibu zoezi la uchanguzi" alieleza Mihayo.

Hivyo aliwataka kutumia vyema mbinu, ujuzi na elimu ya ufundishaji waliyoipata ili kuhakikisha ujumbe uliopo katika mada zitakazowasilishwa unawafikia walengwa kikamilifu pia muweke msisitizo katika kuzingatia taratibu na maelekezo ya muda katika kila hatua hasa kwenye ujazaji wa fomu za ilupigaji kura , kuhesabu na kujumlisha kura ili kutangaza matokeo kwa amani.

Pia aliwataka kuendelea kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na wataalamu wa afya kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Naye Dominicus Lusasi Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mara anaeleza kuwa mafunzo waliyoyapata watayazingitia kikamilifu na kufanya kazi iliyokusidiwa hivyo aliwataka mwenzake kuzingatia maelekezo yote waliyopatiwa sambamba na kuitendea haki serikali.

Aidha mratibu wa mafunzo hayo Mawazo Bikenye anasema wanategemea makubwa baada ya mafunzo hayo na kuwataka wanamafunzo hao kuzingatia yote waliojifunza ili kuleta matokeo mazuri.

Habari Kubwa