Washiriki zaidi ya 500 maonesho ya AZAKI Dodoma

22Oct 2021
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Washiriki zaidi ya 500 maonesho ya AZAKI Dodoma

WIKI ya Asasi za Kiraia (AZAKI), itaanza kesho jijini Dodoma huku washiriki zaidi ya 500 wanatarajiwa kuhudhuria ikiwamo wahisani wa Maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu Wiki ya AZAKI inayoanza Oktoba 23-28, mwaka huu, Mkurugenzi Mkazi wa CBM Tanzania, Nesia Mahenge, amesema wahisani hao wa maendeleo ni pamoja na  Mabalozi Dermark, Uswizi na Canada.

Amesema maonesho hayo  yatakayofanyika viwanja vya Jakaya Kikwete kesho na kesho kutwa na yatafunguliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya  Umoja wa Mataifa(UNA-Tanzania) Reynald Maeda, amesema baada ya maonesho hayo kutakuwa na majadiliano mbalimbali ikiwamo huku miongoni mwa namna AZAKI zinavyochangia kwenye utekelezaji wa Mpango wa tatu wa Maendeleo ya Taifa kwa miaka mitano ambayoa yatafanyikakwa siku tatu kuanzia Oktoba 25 hadi 28, mwaka huu Hoteli ya Royal jijini hapa.

“Kauli mbiu yetu ni mchango wa AZAKI katika maendeleo ya Tanzania na majadiliano yataongozwa na AZAKI wenyewe tukiangalia mchango wa AZAKI kwenye shughuli tunazofanya kazi mbalimbali zinaendaje kusaidia maendeleo ya nchi,”amesema.

Habari Kubwa