Wasiotaka kuchanjwa mnaweza kufa wakati wowote -Rais Duterte

30Jul 2021
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Wasiotaka kuchanjwa mnaweza kufa wakati wowote -Rais Duterte

RAIS wa Ufilipino Rodrigo Duterte, amewaonya raia wake wasiotaka kuchanjwa dhidi ya ugonjwa wa corona kusalia majumbani mwao kwa kuwa hata wakifa yeye hatajali.

RAIS wa Ufilipino Rodrigo Duterte.

Rais huyo amesema watu wanaokataa chanjo wamekuwa ni tisho kwa nchi kwa sababu watakuwa ni wasambazaji wanaotembea wa virusi hivyo.

“Kwa wale watu ambao hamtaki kuchanjwa nawaambia msitoke nyumbani kwenu.Ukitoka nyumbani kwako ,nitawaambia polisi wakurejeshe ndani.”

Utasindikizwa kurejea kwako kwa sababu wewe ni msambazaji unayetembea wa virusi hivi, Iwapo hutaki kuchanjwa basi usitoke kwako, tuwape chanjo wanaozitaka, na wasiotaka kuchanjwa basi mnaweza kufa wakati wowote, MIMI SIJALI”