Watanzania watakiwa kuchukua tahadhari wimbi la tatu Covid-19

20Jun 2021
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Watanzania watakiwa kuchukua tahadhari wimbi la tatu Covid-19

​​​​​​​WIZARA ya Afya nchini Tanzania kupitia Mkurugenzi wa Idara ya Kinga, Dk. Leonard Subi, imewatahadharisha Wananchi wake kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa wa Covid -19 kutokana na kuonekana kwa viashiria vya uwepo kwa wimbi la tatu la mlipuko wa ugonjwa huo, na hiyo ni kufuatia-

-taarifa za ufuatiliaji wa mwenendo wa ugonjwa huo na mwingiliano wa watu kutoka nchi jirani katika shughulia za kiuchumi na kijamii.

Tahadhari hiyo imetolewa na Wizara ya Afya kupitia Mkurugenzi wa Idara ya Kinga, Dk. Leonard Subi, amesema __“Tunakuwakumbusha Watanzania wote kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Covid 19, na tahadhari hii ya leo ni kutokana na hali ya mwenendo wa ugonjwa wa Covid 19 Duniani na ongezeko la maambukizi Afrika zikiwemo Nchi jirani ambazo zimekumbwa na wimbi la tatu la mlipuko wa Covid 19 na maambuki yameongezaka maradufu kuliko ilivyokuwa katika wimbi la pili”

“Kwa mujibu wa taarifa kutoka WHO iliyotolewa katika jarida la wiki ya 24 inayoanzia June 07 hadi June 13, 2021 katika Kanda ya Afrika idadi ya wagonjwa imekuwa ikiongezeka kwa wiki tano mfululizo “

“Mfano katia Wiki moja iliyopita Afrika Kysini, Uganda, Zambia, DRC, Namibia, Angola n.k zimeendelea kuonesha kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa isiyoshuka huku ikiripotiwa Nchi hzio kukumbwa na anuai ya virusi vipya vinavyosababisha Covid 19 kuwa kali zaidi na kuathiri hata mkundi ya wenye umri mdogo”  amesema Dk. Leonard Subi.

 

Habari Kubwa