Watatu wafariki dunia, 88 waugua kipindupindu Katavi

01Jan 2017
Gurian Adolf
Nipashe Jumapili
Watatu wafariki dunia, 88 waugua kipindupindu Katavi

WATU watatu wamefariki dunia na wengine 88 kuugua kipindupindu katika Tarafa ya Karema Ziwa Tanganyika, mkoani humo.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkuu wa wilaya hiyo, Salehe Mhando ilisema ugonjwa huo uligundulika tangu Desemba 9, mwaka jana na mmoja aliugua ugonjwa huo katika kata ya Kapalamsenga akiwa anatoka Kijiji cha Kalya, Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma.

Mhando alisema mlipuko wa kipindupindu umetokea kwenye kata nne zilizopo za Tarafa ya Karema, mwambao mwa ziwa Tanganyika ambazo ni Kapalamsenga, Isengule, Ikola na Karema.

Alisema tangu mlipuko huo, watu 88 wameugua na watatu kati yao wamefariki dunia huku 67 wakipatiwa matibabu katika kambi maalumu zinazotoa huduma ya matibabu ya ugonjwa huo.

Alisema utafiti wa awali umebaini mlipuko huo, umesababishwa na wananchi wa maeneo hayo kutokuwa na vyoo bora na baadhi yao kujisaidia ziwani.

Habari Kubwa