Wateule 75 wa Kikwete waliotemwa hawa hapa

27Jun 2016
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
Nipashe
Wateule 75 wa Kikwete waliotemwa hawa hapa
  • *Mulongo afuata nyayo za Kilango, wanajeshi wapangiwa wilaya zilizopakana na nchi za maziwa makuu

KATIKA kuendelea kukamilisha safu yake ya uongozi, Rais John Magufuli, amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya 139 huku akiwaacha 75 walioteuliwa na mtangulizi wake, Jakaya Kikwete.

Rais john magufuli akiwa ofisini kwake ikulu jijini dar es salaam

Hatua hiyo inatokana na uteuzi wa wakuu wapya 78 huku wawili waliokuwamo katika serikali iliyopita wakiteuliwa kuwa wakuu wa mikoa na Katibu tawala wa mkoa.

Walioteuliwa kuwa mkuu wa mkoa ni Zainab Telack ambaye amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Anne Killango ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Aprili 11, mwaka huu, na Dk. Thea Ntala aliyeteuliwa kuwa katibu tawala wa Mkoa wa Tabora hivi karibuni.

Kabla ya uteuzi huo, Telack alikuwa mkuu wa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza na Dk. Ntala alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Aidha nafasi moja kati ya 78 mpya imejazwa kutokana na kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sarah Dumba.

Uteuzi wa wakuu wa wilaya umefanyika baada ya kukamilika kwa safu za mawaziri, makatibu wakuu na wakuu wa mikoa ingawa pia safari hii amefanya mabadiliko kwenye mikoa miwili.

Katika uteuzi huo, wateule wa Kikwete waliobaki ni 62, kati yao 40 ni aliokuwa amewateua katika awamu yake kuwa wakuu wa wilaya mbalimbali na wengine 22 ni aliokuwa amewateua kuwa wakurugenzi halmashauri za wilaya, ambao Magufuli amewateuwa kuwa wakuu wa wilaya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Rais Magufuli pia ametengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Magesa Mulongo, na nafasi yake itachukuliwa na Dk. Charles Mlingwa.

Hata hivyo, taarifa hiyo haikueleza sababu za kutenguliwa kwa uteuzi huo, ingawa kabla ya Mulongo kuhamishwa kutoka Mwanza na kwenda Mara, alikuwa akiandamwa na kashfa mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kukataa kuishi kwenye nyumba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza tangu alipohamia mkoani humo Desemba, 2014.

Baada ya kutoka Arusha, aliishi hotelini kabla ya kuhamia kwenye nyumba ya kupanga mpaka Novemba, mwaka jana, alipohamia kwenye nyumba ya mkuu wa mkoa.

Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa Said Mwambungu aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu na atapangiwa kazi nyingine na nafasi yake itashikwa na Dk. Binilith Mahenge.

WAKUU WA WILAYA

Katika uteuzi huo, Wilaya za Mikoa ya Kigoma na Kagera ambazo zimekuwa na matukio mengi ya kihalifu, wakuu wa wilaya walioteuliwa kuziongoza wengi ni wanajeshi wenye cheo cha Kanali na Luteni Kanali.

Taarifa hiyo ya Ikulu ilisema moja ya sababu zilizofanya baadhi ya wakuu wa wilaya kuachwa ni pamoja na umri wao kufika miaka 60.

Taarifa hiyo ilimnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, akisema katika uteuzi huo Rais Magufuli amezingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri hasa wenye umri wa zaidi ya miaka 60, ameamua wastaafu.

“Rais amewashukuru sana kwa utumishi wao mzuri na amesema pale ambapo itahitajika, serikali itaendelea kuwatumia katika majukumu mengine,” taarifa hiyo ilieleza.

Aidha, taarifa hiyo ilisema nafasi 78 za wakuu wa wilaya walioachwa zimejazwa na wateule wapya ambao wengi wao ni “vijana, wenye elimu ya kutosha na uzoefu katika maeneo mbalimbali”.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, walioteuliwa kuongoza wilaya za mkoa wa Arusha na wilaya zao kwenye mabano ni Mrisho Gambo (Arusha) huku (Arumeru) Alexander Mnyeti (Ngorongoro) Rashid Taka (Longido) Daniel Chongolo (Monduli), Idd Kimanta (Karatu) na Therezia Mahongo.

Kwa mkoa wa Dar es Salaam Ally Hapi (Kinondoni), Sophia Mjema (Ilala), Felix Lyaviva (Temeke), Hashim Mgandilwa Kigamboni na Ubungo ni Hamphrey Polepole.

Wilaya za Dodoma Vumilia Nyamoga (Chamwino), Christina Mndeme (Dodoma0, Simon Odunga (Chemba), Sezeria Makutta (Kondoa), (Bahi) Elizabeth Simon (Bahi), Jabir Shekimweli (Mpwapwa) na John Ernest Palingo (Kongwa). Mkoa wa Geita ni Josephat Maganga (Bukombe), Martha Mkupasi (Mbogwe), Hamim Gwiyama (Nyang’wale), Herman Kipufi (Geita) na Shaaban Ntarambe (Chato).

Katika mkoa wa Iringa Jamhuri William (Mufindi), Asia Abdallah (Kilolo) na Richard Kasesela (Iringa) wakati Kagera ni Saada Mallunde (Biharamulo), Geofrey Mhelula (Karagwe), Richard Ruyango (Muleba), Kanali Shaban Lissu (Kyerwa), Deodatus Kinawilo (Bukoba), Luteni Kanali Michael Mtenjele (Ngara), Luteni Kanali Denis Mwila (Missenyi).

Mkoa wa Katavi ni Rachiel Kasanda (Mlele), Lilian Matinga (Mpanda) na Saleh Mhando (Tanganyika) na Kigoma ni Samsoni Anga (Kigoma), Kanali Martin Mkisi (Kasulu), Kanali Hosea Ndagala (Kakonko), Mwanamvua Mlindoko (Uvinza), Kanali Elisha Gagisti (Buhigwe) na Luis Bura (Kibondo).

WALIOACHWA

Wakuu wa Wilaya walioachwa na vituo vyao kwenye mabano ni Halima Kihemba (Kibaha), Betty Mkwasa (Mvomero), Muhingo Rweyemamu (Morogoro), Matthew Sedoyeka (Sumbawanga), Jacqueline Liana (Nzega), Benson Mpesya (Songea), Suleiman Kumchaya (Tabora) na Amani Mwenegoha (Bukombe).

Wengine ni Fatma Ally (Mtwara), Jackson Msome (Bukoba), Ramadhani Maneno (Chemba), Hafsa Mtasiwa (Korogwe), Pilly Moshi (Magu), Paul Mzindakaya (Busega), Shabani Kissu (Kondoa), Baraka Konisaga (Nyamagana), Francis Mwonga (Bahi), Gerald Guninita (Kasulu), Omar Kwaangw’ (Karatu), Novatus Makunga (Moshi), Farida Mgomi (Chamwino), Ponsiano Nyami (Bariadi).

Pia wamo Lephy Gembe (Kilombero), Dk. Jacqueline Tiisekwa (Dodoma), Bituni Msangi (Kongwa), Margaret Malenga (Nyasa), Sheni Ngaga (Mbinga), Chande Nalicho (Namtumbo), Agnes Hokororo (Tunduru), Hawa Ng’humbi (Kishapu), Wilson Nkhambaku (Arumeru), Ernest Kahindi (Longido), Francis Mitti (Monduli), Zainab Mlesi (Rungwe), Nyirembe Munasa (Mbeya) na Ahmed Namhone (Mbozi).

Katika orodha hiyo wamo Ziporah Pangani (Igunga), Estherina Kilasi (Muheza), Jowika Kasunga (Mufindi), Khanifa Karamagi (Gairo), Subira Mgalu (Kisarawe), Nurdin Babu (Rufiji), Crispin Meela (Babati), Abdallah Kihato (Mkuranga), Joshua Mirumbe (Bunda) na Ali Mohamed (Serengeti).

Lembris Kipuyo (Rombo), Manju Msambya (Ilemela), Saidi Amanzi (Singida), Lucy Mayenga (Iramba), Kanali Samuel Nzoka (Kiteto), Mahmood Kambona (Simanjiro), Dk. Michael Kadeghe (Mbulu), Yahya Nawanda (Lindi), Charles Gichuri (Ikungi), Christopher Magela (Newala) na Bernard Ndutta (Masasi).

Wengine ni Zuhura Mustapha Ally (Uyui), Khanifa Sirengu (Sikonge), Daudi Yassin (Makete), John Henjewele (Kilosa), Mariam Juma (Lushoto), Husna Msangi (Handeni), Peter Toima (Kakonko), Saveli Maketa (Kigoma).

Pia wamo Rosemary Kirigini (Maswa), Georgina Bundala (Itilima) na Erasto Sima (Meatu), Amina Lugaila (Mbogwe), Ibrahim Marwa (Nyang’wale), Abdulla Lutavi (Tanga), Ephraim Mmbaga (Liwale), Mariam Mtima (Ruangwa), Mariam Mohammed (Lushoto), Selemani Liwowa (Kilindi) na Mboni Mgaza (Kilindi).

www.guardian.co.tz/circulation

Habari Kubwa