Watoto wakike watakiwa kujithamini kuepuka mimba shuleni

15Oct 2020
Christina Mwakangale
Dar es Salaam
Nipashe
Watoto wakike watakiwa kujithamini kuepuka mimba shuleni

WATOTO wa kike wameshauriwa kujithamini na kutambua mabadiliko ya ukuaji ikiwamo kukabiliana na vishawishi vinavyosababisha mimba shuleni.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Sauti ya Mama Africa Foundation (SAMAFO), Tabitha Bugali, aliyasema hao mwishoni mwa wiki ikiwa ni madhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike inayoadhimishwa Oktoba 11, kila mwaka.

Alisema mimba katika umri mdogo kunafifisha ndoto za wasichana, hivyo wapatiwe elimu kutambua haki zao za msingi ikiwamo elimu.

“Sauti ya Mama Africa Foundation ni Asasi isiyo ya Kiserikali, inajihusisha na wanawake na vijana hasa Mtoto wa kike ambaye kutokana na mifumo dume, kandamizi inamnyima haki.

Kwa kulitambua hilo, tunaendesha kutoa elimu kwa vijana walio ndani na nje ya shule kuona mtoto wa kike anajikomboa kielimu ili kufikia ndoto zake,” alisema Bugali.

Pia alisema asasi hiyo inatoa elimu ya ujasiriamali kwa wasichana walea pekee ‘single mothers’ na kuwaunganisha na taasisi zinazoshughulisha kuanzisha vikundi vya kuinuana kiuchumi.

“Wanapokuwa wamejiunga kwenye vikundi wataweza kukopeshwa na halmashauri. kutokana na elimu hii katika shule nyingi tulizopita ufaulu umeongezeka, mimba zimepungua,” alieleza Bugaii.

Alisema kati ya shule zilizopewa elimu hiyo jijini Mbeya ni pamoja na shule ya sekondari Sinde na za msingi Mabatini, Simike na Mbata.

Kauli Mbiu ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike kimataifa ni ‘My Voice, Our Equal Future na kitaifa ni ‘Tumwezeshe Mtoto wa Kike; Kujenga Taifa lenye Usawa’.

Habari Kubwa