Watoto walivyoepushwa kuliwa wanyama wakali

17Jan 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Watoto walivyoepushwa kuliwa wanyama wakali

NDOTO ya miaka mingi ya wanakijiji wa Kakesyo, Tarafa ya Ngorogoro mkoani Arusha kuwa na shule ili kuepusha watoto kuliwa na wanyama wakali kwa kutembea umbali mrefu, imetimia baada ya kuzinduliwa kwa Shule ya Msingi Enyorata Ereko.

Naibu Waziri na Mbunge wa Ngorongoro (CCM) William ole Nasha.

Shule hiyo imejengwa na mwinjilisti Jane Kim (Mama Maasai), raia wa Marekani mwenye asili ya Korea anayefanya kazi ya ujilisti na Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Mount Kilimanjaro (DMK).

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, Naibu Waziri na Mbunge wa Ngorongoro (CCM) William ole Nasha alimshukuru mfadhili huyo.

Ole Nasha alisema ilikuwa ndoto ya miaka mingi ya wakazi hao kuwa na shule kwenye eneo hilo kutokana na watoto wadogo kutembea umbali mrefu kufuata elimu.

“Shule hii itasaidia kuokoa maisha ya watoto dhidi ya wanyama wakali, kukaa muda mwingi darasani tofauti na awali kutembea kilomita 28 hivyo kujikuta wakiwahi kutoka dasarani ili kurudi nyumbani,” alisema.

 

Habari Kubwa