Watu 37 wamelazwa kula chakula chenye sumu msibani

15Dec 2019
Renatha Msungu
Dodoma
Nipashe
Watu 37 wamelazwa kula chakula chenye sumu msibani

WATU 37 wamelazwa katika hospital ya rufani jijini Dodoma baada ya kusadikiwa wamekula chakula chenye sumu katika msiba uliotokea eneo la mtumba lililoko nje kidogo ya jiji hili. 

Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi akiwajulia hali wagonjwa wanaosadikiwa kula chakula chenye sumu katika msiba uliotokea eneo la Mtumba jijini hapa.

Akizungumza hospitalini hapo Meya wa jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe amesema anashukuru jitihada za madaktari wa hospital hiyo waliofanikiwa kuokoa maisha ya watu hao ambao wanahara na kutapika kutokana na kula chakula kinachisadikiwa kuwa na sumu. 

Naye Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobasi Katambi amesema wanasubiri taarifa ya vipimo vya unga na maharagwe yaliyotumika kupikia kwenye msiba huo. 

Amewashukru madaktari wa Hospitali hiyo kutokana na jitihada za huduma ya kwanza iliotolewa kuhakikisha wagonjwa hao wote wamepata Huduma. 

Habari Kubwa