Watu 6 wajeruhiwa na fisi wakati wakimshambulia

28Mar 2020
Marco Maduhu
Shinyanga
Nipashe
Watu 6 wajeruhiwa na fisi wakati wakimshambulia

Watu sita wakazi wa kijiji cha Mwamakalanga Kata ya Samuye wilaya ya Shinyanga mkoani humo, wamejeruhiwa na fisi wakati wakimshambulia kumuua.

fisi.

Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 10 jioni, katika kijiji cha Mwamakalanga wakati Fisi alipovamia kwenye kijiji hicho, ndipo wananchi walipomzingira kumpiga na kusababisha watu hao sita kujeruhiwa .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Deborah Magiligimba , amesema baada ya watu hao kujeruhiwa walikimbizwa hospitali kupatiwa matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri.

Aidha amewataja watu hao kuwa ni Zengo Jitonja, Nkuba Deteba, Juma Salaganda, Limbu Mihambo, Dutu Mdese, na John Matanda.

"Watu hawa wakati wakiwa wamemzingira fisi huyo na kuanza kumshambulia, aliwa ng'ata sehemu mbalimbali za miili yao, ambapo majeruhi watano walipata majeraha madogo na wemeruhusiwa  kutoka hospitali," amesema Magiligimba.

"Majeruhi mmoja Nzengo Jintonja, ambaye alijeruhiwa vibaya kwa kung'atwa mikononi na mdomoni, yeye alikimbizwa kulazwa katika hospitali ya rufani ya mkoa wa Shinyanga na hali yake siyo mbaya sana," ameongeza.

Aidha amesema f isi huyo ameshauawa na wananchi, ambao waliendelea kushambulia kwa kumpiga kwa kutumia zana mbalimbali ikiwamo fimbo. 

Habari Kubwa