Watu milioni 19.6 kati ya milioni 22.9 wamejiandikisha-Jafo

18Oct 2019
Augusta Njoji
DODOMA
Nipashe
Watu milioni 19.6 kati ya milioni 22.9 wamejiandikisha-Jafo

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo amesema watu milioni 19.6 kati ya milioni 22.9 wamejiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, mwaka huu.

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jafo amesema Tamisemi iliweka lengo  la kuandikisha watu milioni 22.9 wenye sifa za kupiga kura na kwamba hao milioni 19.6 waliojitokeza kujiandikisha ni sawa na asilimia 86.

Amesema hakuna mkoa hata mmoja ulioandikisha chini ya asilimia 50, ambapo mkoa wa Dar es salaam umeongoza kwenye uandikishaji kwa asilimia 108,  Pwani 96%, Mwanza 95%, Tanga 93%, Singida 90%, Morogoro 89%, Mbeya 83%, Ruvuma 88%, Katavi 88%, Mtwara 86%, Dodoma 85%, Rukwa 85%, Arusha  85%, Lindi 84%.

Mikoa mingine ni Iringa 84%,  Mara 80%, Kilimanjaro 79%,  Geita 79%, Manyara 79%, Tabora 78%, Songwe 78%, kagera 78%, Shinyanga 76%, Simiyu 76%, Njombe 75% na Kigoma 65%.

Amesema kutokana na kuwepo mafanikio makubwa kwenye uandikishaji huo lile pendekezo alilowasilisha awali kwa Rais John Magufuli la mikoa iliyokuwa ikisuasua kwa sasa atawasilisha dokezo la pongezi kwa viongozi hao waliofanya vizuri.

Habari Kubwa