Watu watano wafariki dunia kwa ajali ya basi Mtwara

16Sep 2020
Hamisi Nasiri
Masasi
Nipashe
Watu watano wafariki dunia kwa ajali ya basi Mtwara

WATU watano wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya gari la abiria aina ya TATA kampuni ya Wite Star linalofanya safari zake kutoka wilayani Masasi kwenda Tandahimba kugongana na basi dogo la Isuzu.

Gari aina Tata , kampuni ya Wite Star linalofanya safari zake kutoka wilayani Masasi kwenda Tandahimba jana limegongana na basi dogo la Isuzu.PICHA : HAMISI NASRI.

Ajali hiyo imetokea jana Septemba 15,2020 majirà ya Saa 7 mchana katika Kijiji cha Msanga Kata ya Mitesa mpakani mwa Wilaya ya Masasi na Newala mkoani Mtwara.

Majeruhi hao sita na miili ya watu waliofariki, walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya Newala.  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mark Njera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwatakà madereva wa vyombo vya moto kuwa waangalifu barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani zinavyowaelekeza.

Habari Kubwa