Watu wenye ulemavu walilia vifaa kujikinga na corona

21May 2020
Enock Charles
DAR
Nipashe
Watu wenye ulemavu walilia vifaa kujikinga na corona

SHIRIKISHO la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) limewaomba wadau mbalimbali kuendelea kuwachangia kupata nakala za vitabu vya nukta nundu na vifaa vingine vya kuwawezesha kupata elimu na kupambana na virusi vya corona.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Shivyawata, Ummy Nderiananga, amesema makundi takriban 10 ya walemavu ambao wanakadiriwa kufika milioni 3 nchi nzima wana mahitaji mbalimbali yanayohitaji msaada wa wadau hasa katika kipindi hiki cha kupambana na janga la corona ikiwamo vitabu hivyo ambavyo vinatoa elimu kuhusu ugonjwa huo.

“Napenda kutumia hadhara hii kuwaomba watu mbalimbali waendelee kutusaidia watu wenye ulemavu hususan kupata vifaa vya kunawia na ‘material’ mbalimbali ambazo inatakiwa watu wenye ulemavu wawe nazo ili kujikinga kama barakoa na vitakasa mikono “ Nderiananga alisema

 

Habari Kubwa