Watumishi 12 matatani kughushi barua za uhamisho

16May 2022
Na Mwandishi Wetu
Nipashe
Watumishi 12 matatani kughushi barua za uhamisho

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Innocent Bashungwa, amemuagiza Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia TAMISEMI Ramadhan Kailim, kuwafuatilia watumishi 12 mkoani Tanga walioghushi barua za uhamisho na kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Innocent Bashungwa.

Waziri huyo ametoa agizo hilo leo Mei 16, 2022 na kutaka warudishwe haraka kwenye vituo vyao vya kazi vya awali.

"Naagiza wote wote waliofanya hivyo watambuliwe kisha Katibu Tawala wa Mkoa awape barua za kuwataka kwa kipindi cha siku tano wawe wamerejea vituo vyao halali kwa gharama zao na iwapo walilipwa pesa za kujikumu (per diem allowance) na usumbufu (disturbance allowance) zilizotokana na uhamisho huo wa kughushi, waelekezwe kuzirejesha ndani ya kipindi cha miezi miwili ya Mei na Juni, 2022""Mamlaka za nidhamu kwenye Halmashauri zao zielekwezwe kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa kosa la kughushi, kuitia hasara Serikali kwa kujipatia fedha (posho ya kujikimu na usumbufu) isivyo halali, kuufanya utumishi wa umma kudharaulika, kwenda kinyume cha maadili ya utumishi wa umma n.k na pia Mamlaka za Usalama, Polisi na PCCB ziwahoji ili wamtaje aliyeghushi saini ili kupata mtandao mzima" amesema Waziri Bashungwa.

Habari Kubwa