Wavumbuzi watakiwa kulinda bunifu zao

20May 2022
Renatha Msungu
DODOMA
Nipashe
Wavumbuzi watakiwa kulinda bunifu zao

KAIMU Mkurugenzi wa Idara ya Miliki Bunifu ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Seka Kasera amewataka wavumbuzi kujijengea utaratibu wa kulinda bunifu zao kisheria kwa kuzisajili ili ziwe salama.

Watumishi wa Brela wakitoa huduma ya usajili kwa wateja waliojitokeza kusajili.

Amesema ili wavumbuzi wawe na uhakika na usalama wa kazi za ubunifu wanazofanya wanapaswa kufuata taratibu za kuzisajili katika mamlaka husika.

“Ulinzi kwa kitu unachokifanya ni muhimu sana hivyo ni vema wavumbuzi kuhakikisha wanasajili na kuweka ulinzi wa bunifu zao kisheria kwa kusajili kwa wakala,”amesema Kasera.

Anafafanua zaidi ya kuwa baada ya kutembelea katika mabanda ya maonyesho yaliyopo katika uwanja huo,wamebaini kuwapo kwa bunifunyingi zenye sifa ya kupata ulinzi ambazo zimebuniwa na vijana wadogo.

"Tumepitia baadhi ya mabanda kuangalia bunifu na ambazo zimepata ulinzi kutokana na kuwa tumezisajili,lakini zipo bunifunyingine zinasifa ya kupata ulinzi ambazo nyingi ni za vijana wadogo ambazo zikipata ulinzi zitaweza kupata soko la kitaifa naKimataifa,"amesema Kasera.

Kutokana na hilo amesema katika maonyesho hayo wanatoa ushauri hivyo amewataka wabunifu wajitokeze kupata usajili kisheria ili kazi zaoziwe salama.

Mbali na hilo Kasera ametoa wito kwa wabunifu ambao wamesajili bunifu zao kuendelea kuziboresha kulingana na mahitaji ya jamii ili ziwe na tija kwao na taifa kwa ujumla.

"Kwa zile bunifu zilizosajiliwa mendeleo endelevu wanajaribu kuziboresha kwa kadri mahitaji ya jamii yanavyohitaji,” amesema Kasera.

"Tangu mwaka 2019,China inaongoza kwa kutoa bunifu nyingi lakini haiongozi kwa kutoa bunifu mpya bali inaongoza kwa kuziongezea uborabunifu za zamani,”amesema. 

Habari Kubwa